Maandamano ya NASA yanoga

 Suleiman Yeri
Maandamano ya NASA yanoga
Maandamano ya kushinikiza kuahirishwa kwa marudio ya kura za urais Alahamisi wiki hii yameanza upya leo baada ya kusitishwa kwa muda ili kutoa nafasi kwa viongozi wa mrengo huo kuzitembelea familia za waliofiwa na waliojeruhiwa wakati wa maandamano hayo.
Wafuasi wa mrengo wa mrengo wa NASA wameandamana katika jiji la, Nairobi, Kisumu na miji mingine huku kauli kuu ikiwa watasusisa uchaguzi na kuirai serikali kuheshimu uamuzi wao.
Licha ya kuandamana kwa amani kutoka Mtaa wa Kondele mjini Kisumu hadi ofisi Tume ya Uchaguzi, IEBC kilitokea kisa ambacho si cha kawaida wakati waandamanji walipowarushia vitoza-machozi maafisa wa polisi waliokuwa wakishika doria katika kituo cha Kondele. Maafisa hao wakilazimika kukimbilia usalama wao.
Uchunguzi wa Radio Maisha umebainisha kuwa vitoza – machozi hivyo ni vile ambavyo wakazi wa eneo hilo wamekuwa wakirushiwa na polisi wakati wa maandamano ya awali bila kulipuka, hivyo wamekuwa wakiviokota na kuhifadhi.
Kwa mujibu wa mmoja wa waandamanaji hao, watafanya kila wawezalo kuhakikisha kuwa marudio ya kura ya urais Alhamisi wiki hii hayafanyiki, hadi kinara wa NASA, Raila Odinga atakapotoa mwelekeo.

Hata hivyo licha yaa maafisa wa polisi kushtumiwa dhidi ya kutumia nguvu kupita kiasi dhidi ya waandamanaji, watu watatu wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Jaramogi Oginga Odinga wakiuguza majeraha mabaya kwa kupigwa na maafisa wa polisi kwenye eneo la Nyawita, Kondele. Afisa Mkuu wa Hospitali hiyo, Dkt. Juliana Otieno amethibitisha kulazwa kwa watatu hao.
Jijini Nairobi, maafisa wa polisi waliwatawanya kwa vitoza-machozi wafuasi wa muungano huo waliokuwa wakiandamana katikati ya jiji licha ya marufuku yaliyotolewa na Waziri Matiang’ia kuwazuia katikati ya miji ya Nairobi, Kisumu na Mombasa kuondeolewa na mahakama wiki iliyopita.
Aidha Seneta wa Siaya, James Orengo amewashtumu mabalozi wa mataifa ya Magharibi waliotoa taarifa kwa vyombo vya habari jana, wakisema serikali ilikuwa imewahakikishia kwamba itaruhusu maandamano yanayofanyika kwa amani.
Akizungumza jijini Nairobi, Orengo amesema ahadi hiyo haijatimizwa leo kwani polisi wameyatatiza maandamano hayo kwenye maeneo mbalimbali nchini yakiwamo yaliyoandaliwa jijini Nairobi.
……………………….

RELATED TOPICS:

Maandamano ya NASA yanoga by: Elie Abi Younes published:

0 Comments

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*

CONTACT US

We're always around to assist you. Kindly send us an email and we'll get back to you, asap.

Sending

©2018 Greezoo

Log in with your credentials

Forgot your details?

Send this to a friend

Skip to toolbar