Maseneta wa NASA walalamika kuhusu uteuzi wa wenyeviti

BeatriceMaganga

Masenetawa NASA walalamika kuhusu uteuzi wa wenyeviti

 Bungela Seneti limeendelea na shughuli ya kuwateua Wenyekiyi wa kamati mbalimbali huku Seneta wa Homabay, Moses Kajwang ambaye ni mwanachama wa Muungano wa NASA akiteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uhasibu wa Umma, PAC huku Mithika Linturi wa Chama cha Jubilee aliteuliwa kuwa naibu wake.

Akizungumzabaada ya uteuzi huo, Kajwang ametoa hakikisho kwamba kamati hiyo itakuwa mstari wa mbele kutekeleza majukumu yake bila miegemeo yoyote, vilevile kufuatilia kwa umakini matumizi ya fedha za kaunti. Kauli sawa na hiyo imetolewa na Linturi ambaye ni Seneta wa Meru.

Hayoyakijiri, Kamati ya Leba ya Seneti & nbsp;inapanga kubuni & nbsp;sheria itakayoruhusu wafanyikazi wa kaunti kuhamishwa kaunti nyingine baada ya kuhudumu kwa muda fulani. Mwenyekiti mpya wa kamati & nbsp;hiyo, Johnson Sakaja amesema iwapo kutakuwa na sheria & nbsp;hiyo itahakikisha usawa na uwiano nchini.

AidhaSakaja amesema ajenda ya kwanza ya kamati yake itakuwa kujadiliana na tume ya kuwaajiri watumishi wa umma kuhusiana na jinsi nafasi za kazi zinavyotangazwa ili kuhakiksha wakenya wote wana nafasi ya kuajiriwa katika utumishi wa umma.

Wakatiuo huo, Mwenyekiti wa Kamati ya Senetiya Uwiano seneta Philip Mpayeei na naibu wake Naomi Jilo wameahidi kuhakiksha wakenya wote wanapatanishwa kupitia ugavi wa nafasi za kazi na raslimali. Aidha katika chaguzi nyingine zilizofanywa & nbsp;leo seneta wa Kiambu Kimani Wamatangi amechaguliwa kuongoza kamati ya uchukuzi na usafiri

Hapojana, Seneta wa Baringo, Gideon Moi aliteuliwa kuwa Mwenyekitiwa Kamati ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia  huku Seneta maalum, Halake Abshiro akichaguliwa kuwa Naibu wake. Senetawa Embu, Njeru Ndwigah alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kilimo huku mwenzake wa Nyandarua, Mwangi Githiomi akichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi na Mali- asili.

Hayoyanajiri huku, maseneta wa Muungano wa NASA wamewashtumu wenzao wa Jubilee kwa madai ya kushirikiana ili kuwafungia nje katika kutwa nafasi za uongozi za kamati mbalimbali za seneti.

Baadhiya maseneta wa NASA akiwamo Seneta wa Kakamega, Cleopas Malala walilazimika kuondoka wakati wa kikao cha kumchagua Mwenyekiti wa Kamati ya Uchukuzi wakidai Ikulu imekuwa na miingilio kuhusu uteuzi huku wakiwashtumu Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto kwa miingilio hiyo.

Senetawa Kiambu Kimani Wamatangi amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchukuzi huku naibu wake akiwa Godana Hargura.

 

 

 

RELATED TOPICS:

.

Maseneta wa NASA walalamika kuhusu uteuzi wa wenyeviti by: Elie Abi Younes published:

0 Comments

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*

CONTACT US

We're always around to assist you. Kindly send us an email and we'll get back to you, asap.

Sending

©2018 Greezoo

Log in with your credentials

Forgot your details?

Send this to a friend

Skip to toolbar