NASA YAIPA MATAKWA IEBC
BY Rosa Agutu
Kuhusumatakwa yaliyotolewa na NASA kabla ya kushiriki uchaguzi ni kwamba matokeo ya urais yatangazwe katika maeneo bunge na kabla matokeo kupeperushwa katika kituo cha kitaifa cha kuhesabia kura. Aidha wanasema ni lazima maajenti wa vyama wapewe fursa ya kuidhimnisha matokeo na kukagua mashine ya kupeperusha matokeo.
Wanasemani sharti Form 34 B zote zichapishwe upya zikiwa na majina ya vituo vya kupigia kura na wagombea. Vilevile maafisa wa kusimamia uchaguzi wa maeneo bunge wanastahili kujaza fomu hizo kwa kalamu kabla ya kutangazwa. NASA inasema hakuna matokeo yatapeperushwa kupitia ujumbe mfupi. Mpangilio huo utashuhudiwa na maajenti wa vyama, vyombo vya habari, waangalizi na umma.
Vilevileimetangaza kuwa uchunguzi wao umeonesha kwamba kind 34 B themanini hazikuwa halali, hivyo kutaka maafisa wa IEBC walioruhusu fomu hizo kutumika kufutwa kazi. Maafisa hao ni Ezra Chiloba, Abdi Guliye, Marijan Hussein Marijan, Betty Nyabuto, James Muhati, Immaculate Kassait, Praxedes Tororey, Moses Kipyegon, Sidney Namulungu, Nacy Kariuki na Silas rotich.
Aidha, viongozi wa NASA wanataka kwamba kabla ya kura kuanza kuhesabiwa saa kumi na moja jioni ni lazima idadi kamili ya walio-piga kura itangazwe kulingana na mashine ya KIEMS.
NASA aidha inataka waatalamu wa kimataifa wasimamie uchaguzi huo huku wakisaidiwa na Tume ya IEBC pamoja na maagenti wa vyama. Muungano huo umesema Jumapili ijayo utaandaa mkutano mkubwa wa kisiasa katika Uwanja wa Jacaranda jijini Nairobi.

ALSO READ: Railastates no election if needs are not fulfilled

NASA YAIPA MATAKWA IEBC by: Elie Abi Younes published:

0 Comments

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*

CONTACT US

We're always around to assist you. Kindly send us an email and we'll get back to you, asap.

Sending

©2018 Greezoo

Log in with your credentials

Forgot your details?

Send this to a friend

Skip to toolbar